WATOTO WADOGO WANATAZAMA PICHA ZISIZOFAA MITANDAONI
Ripoti mpya ya kusikitisha ya Kamishna wa Watoto nchini Uingereza , Dame Rachel de Souza, imefichua kiwango cha kutisha cha watoto kutazama picha na video za ngono mtandaoni.
Ripoti hiyo imetolewa katika uchunguzi wa vijana 1,000 na makundi lengwa yenye vijana wenye umri wa miaka 13 hadi 19.
Ingawa wastani wa umri ambao watoto nchini Uingereza wanaotazama picha na video hizo kwa mara ya kwanza ni miaka 13, uchunguzi ulionyesha kuwa 10% walikuwa wametazama wakiwa na umri wa miaka tisa na zaidi ya robo (27%) walipokuwa na miaka 11.
Moja ya tano ya vijana wa kiume wenye umri wa miaka 16 hadi 21 walikuwa wametazama picha ama video za ngono angalau mara moja kwa siku katika majuma mawili kabla ya uchunguzi.
Hii ni pendekezo la utegemezi ambao hubeba hatari yake ya madhara yanayohusiana," ripoti hiyo inaeeza.
Ripoti hiyo inaonya kwamba maonyesho ya picha za ngono "yameenea na yamefanywa kuwa ya kawaida" na kwamba vijana "mara kwa mara" wanakabiliwa na aina za vurugu zinazoonyesha "vitendo vya ngono vya kulazimisha, vya kudhalilisha au vinavyosababisha maumivu"
Asilimia 79 ya vijana waliohojiwa walikumbana na picha za ngono za kutisha kabla ya kufikia umri wa miaka 18.
Zaidi ya theluthi (38%) walisema waliipata kwa bahati mbaya, lakini nusu ya waliohojiwa (58% ya wavulana na 42% ya wasichana) wenye umri wa miaka 16 hadi 21 walisema waliitafuta.
Zaidi ya robo tatu ya watoto wa miaka 18 hadi 21 walisema machapisho ya ngono kijinsia kabla ya kufikisha miaka 18. Zaidi ya theluthi (36%) ya vijana walisema waliitafuta na ripoti iligundua kuwa unyanyasaji mwingi ulifanywa dhidi ya wanawake. .
Zaidi ya nusu ya wasichana wenye umri wa miaka 16 hadi 21 (51%) walikuwa wametumwa au kuonyeshwa picha za ngono 'iliyojitayarisha' inayohusisha mtu waliyemjua katika maisha halisi, ikilinganishwa na theluthi moja ya wavulana.
Akizungumzia matokeo hayo, Dame Rachel anasema wameweka wazi hitaji la "haraka" la kuchukua hatua kuwalinda watoto dhidi ya madhara ya picha za ngono mtandaoni.
Post a Comment