MTANGAZAJI

ZIARA YA KIONGOZI WA WAADVENTISTA ULIMWENGUNI BARANI AFRIKA

 



Kiongozi wa Kanisa la Waadventista wa Sabato Duniani Ted Wilson yuko barani Afrika katika ziara maalum akiambatana na Mkewe Nancy ambapo  mpaka sasa ameshatembelea Zambia na Kenya huku akitarajiwa kuzitembelea nchi za Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kabla ya kumalizika kwa juma hili.

Akiwa nchini Zambia kwa takribani juma moja Ted alikutana na Rais wa nchi hiyo Hakainde  Hichilema ambaye ni Muumini wa Kanisa la Waadventista wa Sabato  Ikulu jijini Lusaka na kisha akatembelea baadhi ya Taasisi za kanisa hilo nchini humo ikiwemo Shule ya Sekondari ya Rusangu na Riverside,Chuo Kikuu cha Mulungushi, Hope Channel Zambia na Kituo cha Radio Maranatha 

Nchini Kenya Ted Wilson amefanya mazungumzo na Rais wa Kenya William Ruto  katika Ikulu ya nchi hiyo Februari 5,mwaka huu na kisha kuhutubia maefu ya waumini wa Kanisa hilo huko Nakuru Februari 6,2023 

Kiongozi huyo anatarajiwa kuwahutumia maelefu ya waumini wa Kanisa la Waadventista nchini Tanzania Februari 8,mwaka huu katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Wilson ambaye utakuwa ni muhula wake wa tatu sasa kuongoza Kanisa la Waadventista wa Sabato Ulimwenguni , alichaguliwa kuwa kiongozi wa Kanisa la Wa Adventista wa Sabato Ulimwenguni kwa mara ya kwanza katika Kikao cha Konferensi Kuu ya 2010, akichukua nafasi ya Jan Paulsen, ambaye alihudumu katika nafasi hiyo  tangu 1999. Mnamo mwaka 2015, katika Kikao cha 60 cha Mkutano Mkuu, Wilson alichaguliwa tena kwa muhula wa pili wa miaka mitano.


Ted N.C. Wilson  anayezungumza Kiingereza,Kifaransa na Kirusi ni Mtoto wa aliyekuwa Kiongozi wa Kanisa la Wa Adventista wa Sabato Ulimwenguni Neal C.Wilson 1979 hadi 1990,  amehudumu katika  Kanisa la Wa Adventista  wa Sabato kwa  majukumu mbalimbali kwa  miaka 50. Alianza akiwa  mchungaji katika Konferensi ya The Greater New York mnamo 1974, na baadaye akahamia katika majukumu ya kiutawala na huduma za kigeni.


Amewahi kuwa Kiongozi wa Kanisa la Wa Adventista wa Sabato katika Divisheni ya Trans Euro Asia makao yake makuu yakiwa Moscow Urusi mwaka 1992 hadi 1996,kabla ya hapo akifanya kazi katika Divisheni ya Afrika na Bahari ya Hindi huko Abidjan Ivory Coast hadi mwaka 1990 ambapo alikuwa Mkurugenzi wa Idara na Katibu Mtendaji.Amewahi pia kuwa Mkurugenzi na baadaye Katibu Mtendaji kwenye Ofisi za Makao Makuu ya Kanisa la Wa Adventista wa Sabato zilizopo Silver Spring Maryland Marekani.


Wilson ana shahada ya Udaktari wa Falsafa katika Elimu ya Dini kutoka Chuo Kikuu cha New York,Shahada ya Uzamili ya elimu ya Uungu kutoka Chuo Kikuu cha Andrews, na Shahada ya Uzamili ya Sayansi katika Afya ya Umma kutoka Chuo Kikuu cha Loma Linda.

Akiwa Loma Linda  alikutana na mke wake, Nancy, mtaalamu wa tiba ya viungo, na kwa pamoja wamefanikiwa kupata watoto  watatu, Emilie, Elizabeth, na Catherine.



No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.