MTANGAZAJI

APIGWA RISASI AKIWA KANISANI

 


Mwanachama wa genge  la wahalifu la  Mongrel, Daniel Eliu, 46 amepigwa risasi nje ya Kanisa la Waadventista la Papatoetoe Aucklanda New Zealand siku ya Sabato  Desemba 17 mwaka huu katika kile polisi wanachokiita shambulizi lililolengwa.
Eliu alikuwa akihudhuria kanisani hapo katika mkutano maalum ulioopewa jina la True Stories ulioendeshwa  na taasis ya Grace  inayolenga kuboresha maisha ya watu kutoka malezi yaliyotengwa kwa lengo la kubadilisha maisha yao. 
Watu waliokuwa ndani wanasema walisikia sauti za kishindo na hawakutambua kilichotokea hadi walipomwona Eliu akiwa amedondoka nje,ameeleza David Letele mkuu wa Taasisi ya Grace,aliyejaribu kumwokoa kwa huduma ya dharura lakini Eliu hakunusurika. 
Waumini walikusanyika katika kanisa la Papatoetoe kwa ibada ambayo ilichelewa kwa sababu ya tukio hilo.
Phillip Barber, ambaye alikuwa ndani ya kanisa hilo wakati wa tukio, aliiambia Newshub ya New Zealand  kwamba uvumi ulianza kuenea kwamba kuna kitu kinatokea nje. Waliambiwa wasiondoke kwenye eneo hilo.
Inspekta wa upelelezi Tofilau Faamanuia Va'aelua anasema ufyatuaji risasi huo unaonekana kuwa tukio la pekee, kwani mwathiriwa alilengwa kimakusudi.
Polisi wanafuata njia chanya za uchunguzi kumtafuta mhalifu, na watu waliokuwepo kanisani wanasaidia polisi katika uchunguzi wao, anasema.
Picha kutoka eneo la tukio zilionyesha wanachama  wengi wa Mongrel Mob nje ya kanisa baada ya tukio, pamoja na washiriki waliochanganyikiwa,magari 25 ya polisi yalijitokeza kwenye eneo hilo baada ya tukio hilo.
Letele, kutoka Taasisi ya  Grace, alichapisha kwenye mitandao ya kijamii akiomba "amani na utulivu katika wakati huu mgumu," akiwahimiza wanachama wa magenge "kuacha vumbi la janga hili litulie."

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.