"AGENDA" YA UTOAJI MIMBA YASABABISHA UADUI KWA WAKRISTO MAREKANI
Angalau vitendo 420 vya uadui dhidi ya makanisa vilitokea nchini Marekani katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, uchambuzi unapendekeza.
Takriban vitendo 57 kati ya hivyo vya uhasama vilitokea kati ya Januari na Septemba 2022 na vilihusiana na mitazamo kuhusu utoaji mimba.
Ripoti mpya ya Baraza la Utafiti wa Familia (FRC), shirika la Kikristo la wanaharakati wa kihafidhina lililoko Washington, lilichanganua data inayopatikana hadharani kati ya Januari 2018 na Septemba 2022 ili kuandika vitendo vya uhasama vinavyolengwa katika makanisa 397 ya majimbo 45 ya Marekani na Washington, D.C.
Vitendo hivyo ni pamoja na uharibifu, uchomaji moto, matukio yanayohusiana na bunduki na vitisho vya mabomu. Ripoti inatanabaisha kwamba mitazamo mikali mashambulizi ya mara kwa mara kama hayo yanaweza kutishia jumuiya ya Kikristo.
Ripoti inaonesha kuwa Mnamo mwaka 2018, kulikuwa na visa 50 vya uhasama dhidi ya makanisa, mwaka 2019, idadi hiyo iliongezeka hadi 83 na kupungua hadi 54 mnamo mwaka 2020 huenda ni sababu ya vizuizi vya serikali wakati wa janga la uviko-19.
Mnamo 2021, kulikuwa na matukio 96 ya uhasama dhidi ya makanisa, na kati ya Januari na Septemba 2022, kulikuwa na 137.
Kwa mfano, Machi 2022, jengo la Kanisa la KiBaptist huko Bartow, Florida, liliharibiwa katika shambulio la kuchomwa moto. Kanisa la Journey la Sonora huko California pia liliharibiwa katika shambulio la uchomaji moto mwezi Machi.
Julai, moto ulianza katika makanisa mawili huko Maryland,Washington, D.C.—Kanisa la Methodist la Kaskazini Bethesda na la Jane Frances la RC la Montgomery, kanisa la tatu lililo karibu la Kibaptist la Bethesda Wildwood liliharibiwa.
Ripoti hiyo inaongeza kuwa majimbo yenye idadi kubwa ya watu yalielekea kuripoti matukio zaidi. California ilikuwa na matukio mengi zaidi, ikiwa na matukio 51. Texas matukio 33, New York 31 na Florida 23. Delaware, Montana, Nebraska, New Hampshire na Vermont ndio majimbo pekee ya Marekani ambayo hayakuwa na matukio yanayojulikana wakati wa uandaaji wa ripoti hiyo.
Post a Comment