MTANGAZAJI

BAADHI WACHUKIZWA NA RIPOTI YA MWANZO YA MAUAJI YA WANAFUNZI



 
Makosa  ya kibinadamu yameelezwa kuwa  yalichangia pakubwa katika kushindwa kutekeleza sera za dharura katika Shule ya Msingi ya Robb, kulingana na wataalamu wa haki ya jinai na usalama wa shule ambao walichambua ripoti kuhusu ufyatuaji risasi shuleni hupo Uvalde, Texas.
 
 Kamati ya Bunge la Texas Jumapili imetoa ripoti ya awali yenye karibu kurasa 80 kulingana na mahojiano na zaidi ya mashahidi 30, pamoja na rekodi za sauti na video kutoka eneo la tukio. Huu ni uchanganuzi thabiti zaidi uliochapishwa kuhusu ufyatuaji risasi katika shule ya hiyo  Mei 24,2022.
 
 Wataalam wameviambia vyombo vya habari kuwa ingawa idara ya Polisi ya shule na ya wilaya walikuwa na sera na mafunzo ya jinsi ya kukabiliana na wapiga risasi, walishidwa kusimamia kwa vitendo kwa sababu ya makosa ya kibinadamu.
 
 Baadhi ya wapendwa wa wahasiriwa na wanajamii huko Uvalde,Texas wamejibu kwa hasira na kukatishwa tamaa, hasa kwa maelezo ya jinsi maofisa walivyosubiri kuingia darasani la shule hiyo.
 
“Inachukiza. Inachukiza, "amesema Michael Brown, ambaye mtoto wake wa miaka 9 alikuwa kwenye mkahawa wa shule siku ya kupigwa risasi na kunusurika. "Wao ni waoga."
 
Taarifa za uchunguzi zilizoandikwa na mtandao wa USA Today zinaonesha kuwa  Shule ya Msingi ya Robb ilikuwa na "utamaduni wa kusikitisha wa kutofuata sheria" kati ya wafanyakazi wa shule katofunga kufungua milango na kufuli. Hakuna mtu aliyekuwa amefunga milango mitatu ya nje ya jengo la magharibi mwa shule, ukiukaji wa moja kwa moja wa sera ya shule, ripoti inasema.


No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.