KIONGOZI WA DINI ASHTAKIWA KWA UTAKATISHAJI WA FEDHA
Aliyekuwa Mkuu wa Operesheni katika Dayosisi ya Anglikana ya London ameshtakiwa kwa ulaghai na utakatishaji fedha kutokana na madai ya upotevu wa zaidi ya dola milioni 5.9 (pauni milioni 5) kutoka kwa Dayosisi hiyo kati ya 2009 na 2019.
Martin Sargeant, mzee wa miaka 52 ambaye alikuwa mkuu wa shughuli za Mfuko wa Dayosisi ya London (LDF) jijini London na Westminster ameshtakiwa kwa udanganyifu ambao unaelezwa kuwa ni wa kihistoaria katika taasis hiyo ya dini.
Sargeant aliondoka katika Dayosisi hiyo, inayojumuisha parokia, shule, makasisi, jumuiya za kimisionari na mashirika mengine, mwaka 2019 baada ya Askofu mpya wa London, Mchungaji Sarah Mullally, aliomba jukumu lake liangaliwe upya.
Taarifa kutoka Dayosisi inasema "Wakati huo hapakuwa na tuhuma au ushahidi wa uhalifu, lakini mwaka jana, LDF ilitoa ripoti kwa kitengo cha Polisi kinachoshughulikia Udanganyifu na utakatishaji wa fedha na ripoti ya tukio kubwa kwa Tume ya Misaada, baada ya parokia kuibua wasiwasi kuhusu fedha ambazo walikuwa hawajapokea.
Mullally anasema LDF "ilifanya kazi bila kuchoka na polisi katika mwaka uliopita Jumla ya pesa zinazohusika inaaminika kuwa kiasi cha Pauni milioni 5 za Uingereza zinazohusika na mashirika tofauti.
Post a Comment