MTANGAZAJI

SHIRIKA LA POSTA TANZANIA LATAKIWA KUWA NA UBUNIFU WA KIBIASHARA

 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano),
Dkt. Jimmy Yonazi akizungumza kabla ya uzinduzi wa huduma ya uwakala baina ya Shirika la
Posta Tanzania na Benki ya Watu wa Zanzibar uliofanyika kwenye ukumbi wa VETA,
Dodoma. Wanaomsikiliza wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Idd
Haji Makame na anayefuata ni Hassan Mwang’ombe, PostaMasta Mkuu wa Shirika hilo.

Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Hassan Mwang’ombe (aliyeketi kushoto) na
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ), Idd Haji Makame (aliyeketi
kulia), wakitia saini Mkataba wa ushirika wa kutoa huduma za kifedha baina ya Shirika hilo
na Benki ya PBZ. Aliyesimama nyuma mwenye tai ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Mwinyi Talib Haji pamoja na baadhi
ya watendaji wakishuhudia tukio hilo.

 

 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Dkt Jimmy Yonazi amelitaka Shirika la Posta Tanzania (TPC) kujiendesha kibiashara katika sekta ya Mawasiliano.
 
Agizo hilo amelitoa wakati wa uzinduzi wa  uzinduzi wa huduma za Uwakala, baina ya Shirika hilo na Benki ya Watu wa Zanzibar uliofanyika kwenye ofisi za Posta mjini Dodoma.

Yonazi ameeleza kuwa TPC ni taasisi inayofanya vizuri chini ya Sekta ya Mawasiliano kwa hivyo wanapaswa  kuwa wabunifu kujiendesha kibiashara, na kwa ushirika huo utaletamwanga mpya kwa huduma za posta na huduma za fedha nchini Tanzania na kuwa mfano kwa mataifa mengine ambapo ametoa rai kwa taasisi hizo kuhakikisha kuwa mataifa mengine ya Afrika yanajifunza kutoka kwao na kutumia ubunifu wa aina hiyo .
 
Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya PBZ, Idd Haji Makame,amesema kuwa utoaji wa huduma za PBZ kupitia Shirika la TPC utakuwa rahisi na nafuu kwasababu shirika la TPC lina mtandao mpana na linapatikana kila mahali nchi nzima huku kwa upande mwingine ushirika huu utaifanya PBZ ijulikane na kuwafikia wateja wengi zaidi.

Naye Postamasta Mkuu wa Shirika la TPC, Hassan Mwang’ombe amesema kuwa ushirikahuu wa uwakala wa PBZ ni mwendelezo wa Shirika lake la TPC katika kutimiza ndoto za kuwa kituo cha kutoa huduma mbalimbali mahali pamoja ili kuwawezesha wateja wa Shirika hilo na wananchi kupata huduma za aina mbali mbali mahali pamoja (one stop centre) ili kuwarahisishia wananchi kupata huduma na waweze kuokoa muda wao badala ya kutafuta huduma kwenye ofisi au taasisi tofauti ambapo itawawezesha kuendelea na shughuli
nyingine za kiuchumi na kijamii.

Mwang’ombe amesema kuwa Shirika lake la TPC limeunganishwa na mashirika mengine ya posta yapatayo 660 ulimwenguni kote ambapo ushirika baina yao na PBZ utatoa fursa kwa wateja wao kutumia huduma za uwakala na huduma nyingine za TPC ndani na nje ya Tanzania

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.