WIZARA YA MALI ASILI NA UTALII KUTUMIA MFUMO WA KIELEKITRONIKI KWA WAGENI WA NDANI NA NJE YA TANZANIA
Baadhi ya Wamiliki wa Huduma za malazi wakifuatailia mafunzo ya usajili wa Wageni kwenye mfumo wa MNRT PORTAL |
Wageni wa ndani na nje ya Tanzania watakaolala kwenye
Huduma za Malazi zilizosajiliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa
mujibu wa sheria kuanzia Oktoba 1, 2020 watatakiwa kuanza kusajiliwa
kwenye mfumo wa kielekitroniki wa MNRT PORTAL.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya
Utalii, Philip Chitaunga ametoa taarifa hiyo jijini Dar es salaam wakati alipokuwa akifungua mafunzo ya siku
moja ya Usajili Wageni wanaolala kwenye Huduma za Malazi kupitia mfumo
wa kielektoniki wa MNRT PORTAL kwa Wamiliki wa Malazi wapatao 200 wa
Kanda ya Pwani.
Amesema
lengo kuu la kusajili Wageni hao katika huduma hizo ni kupata taarifa
zitakazosaidia Serikali kupata takwimu sahihi kwa ajili ya kuboresha
sekta ya Utalii nchini.
Amesema
taarifa hizo zitatumika kama nyezo katika kuandaa sera,mikakati na
mbinu katika kuboresha sekta ya utalii hasa utalii wa ndani ambao
mwamko wake umekuwa mdogo kwa Wananchi
Mfumo huo wa kusajili wageni utatumika katika Hoteli, Kambi pamoja na Loji pekee zinazotambulika na Wizara hiyo
Amesema
utaratibu huo wa kusajili Wageni ni takwa la kisheria, Hivyo amewataka
Wamiliki wa Malazi hao kuhakikisha kuanzia tarehe 1, Oktoba mwaka huu
wanaanza kutekeleza agizo hilo kwa kusajili Wageni wanaofika katika
Huduma za malazi kwa kutumia vitambulisho hivyo.
Katika
hatua nyingine, Kaimu Mkurugenzi, Chitaunga amewatoa hofu Wamiliki wa
malazi kuwa taarifa hizo za Wageni zitatumika kwa ajili ya matumizi ya
serikali pekee na zitatunzwa kwa usiri wa hali ya juu.
Kwa
upande wake, Samson Nelsa ambaye ni mmiliki wa Huduma za Malazi katika
mkoa wa Pwani, amesema mfumo huo utasaidia serikali kuandaa takwimu za
idadi ya watalii
Amesema
mfumo huo mbali ya kuisaidia Serikali kupata takwimu za utalii wa ndani
na wa nje pia utasaidia Wamiliki wa Hoteli kuwa na sehemu salama ya
kuhifadhia taarifa zao.
Naye Mohamed
Juma ambaye ni mmiliki wa Hoteli ya Rainbow licha ya kuipongeza Wizara
ya Maliasili na Utalii kwa kutaka kuwa na takwimu halisi za watalii
kupitia mfumo huo utakaoanza kutumika mwezi ujao ameitaka Wizara hiyo
kuwa ihakikishe hakuna taarifa za wateja wao zinatumika kwa ajili ya
maslahi binafsi
Pia Ameitahadhalisha Wizara
kuwa makini katika kuulinda mfumo huo ili usiweze kudukuliwa na baadhi
ya watu kwa ajili ya maslahi yao binafsi.
Post a Comment