MTANGAZAJI

WHISPERING HOPE:KUNDI LA UIMBAJI LINALOIMBA NYIMBO KWA KISWAHILI NCHINI MAREKANI (+VIDEO)

Whispering Hope ni Kundi la nyimbo za Injili lililoko jijini Houston,Texas nchini Marekani ambalo linaimba nyimbo za Injili kwa Lugha ya Kiswahili.

Kundi hilo lenye waimbaji toka Tanzania,Kenya,Jamaica na Nigeria linatoka katika Kanisa la Waadventista wa Sabato la Houston International.

Miongoni mwa waimbaji wa Kundi hilo ni mwimbaji wa sauti ya kwanza Joy Frerking ambaye alikuwa mwimbaji katika Kwaya ya Kanisa la Waadventista wa Sabato Magomeni Mwembechai jijini Dar es salaam,Tanzania kabla ya kuhamia Marekani.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.