MTANGAZAJI

KWAYA YA INJILI FAMILY TOKA DRC WAENDELEA KUWEPO NCHINI TANZANIA (+VIDEO)



Waimbaji wa Kwaya ya Injili Family toka Goma,DRC wameendelea kuwepo nchini Tanzania kwa juma la pili sasa ikiwa ni ziara yao ya kutoa huduma ya uimbaji kwenye mikutano  Makambi kwa mwaka huu.

Wakianzia Jijini Arusha kwa Mkutano wa Makambi ya Kanisa la Waadventista wa Sabato Burka juma lililopita ambako pia walishiriki katika uzinduzi wa Santuri ya Waimbaji wa Kwaya Kongwe ya Burka,Juma hili wapo katika Mkutano wa Makambi unaofanyika Dodoma Kati na watahitimisha ziara yao kwa Makambi yatakayofanyika juma lijalo Agosti 25-Septemba 1,2019  Ukonga jijini Dar es salaam.


Injili Family ni Kwaya ya Kanisa la Waadventista wa Sabato nchini DRC iliyoanzishwa mwaka 1985 ikiwa na mafanikio ya kusaidia kuanzishwa kwa kwaya zingine zaidi ya 100 jijini Goma.



-->

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.