MTANGAZAJI

KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO KUTOA HUDUMA ZA AFYA BURE JIJINI MWANZA MWEZI HUU


Kanisa la Waadventista Wa Sabato nchini Tanzania litaendesha huduma ya upimaji wa Afya na Matibabu bure katika uwanja wa CCM Kirumba wakati wa mkutano wa Ufunuo wa Matumaini kuanzia Mei 12 hadi juni 2 mwaka huu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Afya ya Mkutano huo Mfamasia toka Hospitali ya Rufaa ya Bugando John Pemba ameiambia blog hii kuwa wameamua kutoa huduma hizo ili kuigusa jamii ya wananchi wa mikoa ya kanda ya ziwa ikiwa ni sehemu ya mkutano huo katika kuifikia jamii

Ameleza kuwa watapima na kutoa ushauri nasihi kwa magonjwa ya Kisukari,tezi dume,saratani ya mlango wa kizazi na VVU ambapo wataanza kutoa huduma hizo kila siku kuanzia saa nne asubuhi hadi saa 10 jioni.

Masuala ya Afya ni sehemu ya utume wa kanisa la waadventista Wa Sabato ulimwenguni katika kuifikia jamii katika mahitaji yake.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.