MTANGAZAJI

ZABRON SINGERS KUTOA HUDUMA YA NYIMBO KATIKA GEREZA KUBWA JIJINI NAIROBI,KENYA

Zabron SIngers katika kanisa la Thigio

Waimbaji wa Nyimbo za Injili ambao ni ndugu toka Kahama Shinyanga,Zabron Singers wako katika ziara ya kutoa huduma ya uimbaji huko nchini Kenya.

Kuanzia Mei 28  mpaka Juni 10 mwaka huu watakuwa wakitoa huduma ya uimbaji kwenye Gereza la Wanawake lililo kubwa kuliko yote  nchini Kenya (LANG'ATA WOMEN PRISONS) lililopo Nairobi.
 
Kabla ya hapo walishiriki katika mkutano wa Injili uliofanywa na kanisa la Waadventista Wa Sabato  Thigio,Limuru.
 
Zabron Singers wanatoka katika familia ya Marehemu  Zabron ambaye alikuwa Mtunzi,Mpiga gitaa na Mwanzilishi wa Kwaya ya Kagunga iliyoko Sengerema,Mwanza Tanzania.
 
Miongoni mwa matoleo yao ya nyimbo ni Nawakumbuka na Mkono wa BWANA,huku  nyimbo zao zinazofahamika zikiwa ni Asikucheleweshe na Shigongo walioimba kwa lugha ya Kisukuma miongoni mwa makabila zaidi ya 120 yanayopatikana nchini Tanzania.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.