DAR ES SALAAM:PICHA SABA ZA NDEGE ILIYONUNULIWA NA SERIKALI YA TANZANIA ILIPOWASILI HII LEO
Ndege iliyonunuliwa na Serikali kwa ajili ya kutumiwa na
Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) imetua katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam ikitokea nchini Canada
ilikotengenezwa.
Ndege
hiyo aina ya Bombadier Q400 NextGen imetua majira ya saa 6:15 Mchana leo na
kisha kupatiwa heshima maalum ambayo hutolewa kwa ndege yoyote mpya
inayotua katika nchi yake (Water Salute).
Baada ya kupokea heshima hiyo, ndege imeegeshwa katika eneo la ndege za jeshi (Airwing Ukonga).
Akizungumza
baada ya kuwasili kwa ndege hiyo Katibu Mkuu Uchukuzi Dkt. Leonard
Chamriho amesema ndege ya pili inatarajiwa kuwasili baada ya wiki moja
na kwamba baada ya kuwasili ndege ya pili ndipo yatafanyika mapokezi
rasmi, yatakayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli kwa tarehe itakayotangazwa baadaye.
Post a Comment