MTANGAZAJI

DAR ES SALAA:WAIMBAJI WA THE LIGHT BEARERS WAELEKEA READING,UINGEREZA

Waimbaji wa The Light Bearers wakiwa katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere muda mfupi kabla ya kuondoka hii leo

 

Baadhi ya Marafiki waliokuwepo uwanjani hapo

Waimbaji 14 wa The Light Bearers toka JCB Studioz za jijini Dar es salaam wameondoka hii leo Agosti 4,Mwaka huu kuelekea Reading,Uingereza kuimba katika Mkutano wa Injili wa majuma matatu ambao utaendeshwa na Kanisa la Waadventista Wa Sabato la Angaza la mjini humo.

Mkutano huo wa Injili utaendeshwa na Mchungaji Baraka Butoke ambaye aliwahi kuishi na kulelewa na Kanisa la Angaza nchini Uingereza wakati akiwa kijana mdogo.

Kiongozi wa The Light Bearers Waziri Barnabas ambaye ameongozana na waimbaji hao amesema safari hiyo ni fursa na nafasi nyingine ambayo Mungu amewapatia kuhudumu kwa njia ya nyimbo za Injili nje ya mipaka ya Tanzania.

Kanisa la Angaza limekuwa na utaratibu wa kuwaalika waimbaji toka wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Tanzania kwenda kushiriki kwenye mikutano ya Injili nchini humo kuanzia mwaka 2004.

The Light Bearers mpaka sasa wanamatoleo manne ya audio huku matoleo mawili yakiwa yanasubiriwa kutambulishwa hivi karibuni katika vyombo vya habari nchini Tanzania.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.