MTANGAZAJI

DAR ES SALAAM:WATANZANIA WALIOSOMA BUPANDAGILA WAKUTANA KUJADILI JINSI YA KUISAIDIA SHULE HIYO




Watanzania waliosoma katika shule ya Sekondari ya Bupandagila inayomilikiwa na Kanisa la Waadventista Wa Sabato leo wamefanya kikao cha kwanza jijini Dar es salaam kwa ajili ya kuweka mikakati ya kusaidia shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 1983.

Wazo la kuisaidia shule hilo limeanzishwa na watanzania hao kupitia mtandao wa kijamii wa WhatsApp ambapo sasa kuna jumla ya watu 79  na wengine ambao hawako kwenye jukwaa  hilo walioko nchini na nje ya nchi.

Shule hiyo inayomilikiwa na Kanisa la Waadventista Wa Sabato nchini Tanzania iko wilayani Bariadi,Mkoani Simiyu.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.