MTANGAZAJI

DAR ES SALAAM:WAIMBAJI WA KWAYA YA NYEGEZI YA JIJINI MWANZA WAWASILI JIJINI DAR ES SALAAM KUHUDUMU KATIKA MAKAMBI MAWILI

 

 Waimbaji wa Kwaya ya Waadventista Wa Sabato ya Nyegezi jijini Mwanza wamewasili jana jijini Dar es salaam,kwa ajili ya kutoa huduma ya Uimbaji kwenye Mkutano wa Makambi ya Magomeni yaliyofunguliwa leo.

Kwaya hiyo ambayo kwa sasa inatoleo lake jipya la Santuri Mwonekano iitwayo Utukuzwe itahudumu pia kwenye Makambi ya Mtaa wa Pugu juma moja lijalo,kabla ya kuja Dar es salaam waimbaji hao pia walishiriki kwenye makambi ya Mbauda jijini Arusha.

Kanisa la Waadventista Wa Sabato Duniani kote huwa na utaratibu wa mikutano ya Makambi kwa mujibu wa Biblia ambao hufanyika kwa muda wa siku saba kati ya mwezi wa saba hadi wa tisa kwa kila mwaka.

Kipindi cha Lulu za Injili kupitia Morning Star Radio cha siku ya jumamosi kimefanya mazungumzo na baadhi ya waimbaji wa kwaya ya Nyegezi  

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.