MTANGAZAJI

THE LIGHT BEARERS TOKA TANZANIA WAIMBA KWA MARA YA KWANZA KWENYE IBADA YA SABATO NCHINI UINGEREZAMchungaji Baraka Butoke akitoa fundisho kwa Watoto wakati wa IbadaWaimbaji wa The Light Bearers toka Tanzania leo wameimba kwa mara ya kwanza katika Ibada ya Sabato iliyoendeshwa na Kanisa la Waadventista Wa Sabato la Angaza lililoko Reading nchini Uingereza ambako watadumu kuwepo nchini humo kwa muda wa majuma matatu katika mkutano wa Injili unaoendeshwa na Mchungaji Baraka Butoke toka Tanzania.

Kiongozi wa LB na Mkurugenzi wa JCB Studioz Waziri Barnabas ameiambia wavuti hii kuwa huduma yao imeonekana kupokelewa vyema na waumini wa Kanisa la Angaza pamoja na wasio waadventista wanaotoka katika nchi za Afrika Mashariki na Kati.

Waziri pia amezungumzia mabadiliko ya masaa kati ya Uingereza na Tanzania na kueleza kuwa hilo nalo limewapa changamoto ya kuendana na mabadiliko ya hali ya hewa yaliyopo katika nchi hiyo hasa siku ya jana baada ya kuendelea kuliona jua wakati ikiwa ni saa tatu za usiku jambo ambalo ni tofauti kwa majira ya Afrika Mashariki.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.