DAR ES SALAAM:JAJI MKUU MOHAMED CHANDE OHMAN KUWA MGENI RASMI KATIKA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI

Mwenyekiti
wa MISATAN, Simon Berege akizungumza na waandisshi wa habari kuhusu
SIku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari. Kushoto ni Afisa Mafunzo wa TMF,
Raziah Mawanga na Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Jamhuri na Makamu
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Deodatus Balile.(Picha na Modewjiblog)
Siku
za Uhuru wa Vyombo vya Habari ambayo hufanyika Mei 3 ya kila mwaka
inataraji kufanyika jijini Mwanza kwa mwaka huu ambapo mgeni rasmi
anatarajiwa kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman na
kuhudhuliwa na viongozi wengine nchini na wengine kutoka nje ya nchini
ambapo kwa mwaka huu kaulimbiu ni KUPATA TAARIFA NI HAKI YAKO YA MSINGI.
Akizungumzia
sherehe hizo katika mkutano na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa
MISATAN, Simon Berege amesema sherehe za mwaka huu zinataraji kuwa na
wageni zaidi ya 250 akiwepo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Mhe. Nape Nnauye, Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini,
Alvaro Rodriguez na Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa
Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira
Rodrigues.
Berege amesema kuwa siku ya uhuru wa vyombo vya habari kwa mwaka huu
itafanyika kwa siku mbili, Mei, 2 kutakuwa na kongamano ambalo
litatumika kujadili hali ya uhuru wa vyombo vya habari nchini na Mei, 3
ndiyo itakuwa siku husika ya maadhimisho.
“Kikawaida
huwa kuna mambo tunafanya katika siku hiyo, tutawakumbuka waandishi wa
habari waliopoteza maisha kazini, tutawakumbuka waandishi wa habari
maveterani na waandishi wa habari waliopatwa na matatizo wakiwa kazini
... kwa mwaka huu tutakuwa na mambo ya kipekee tofauti na miaka
iliyopita,” amesema Berege.
Pia
ameongeza kuwa watapitia sheria zinazohusu uhuru wa vyombo vya habari
kama Cyber Crime Act 2015 na Sheria ya Takwimu 2015 pia kuipitia miswada
ya huduma ya vyombo vya habari na uhuru wa kupata taarifa.

Mhariri
Mtendaji wa Gazeti la JAMHURI na Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la
Wahariri (TEF), Deodatus Balile akizungumzia hali ya uhuru wa vyombo vya
habari na haki ya kupata taarifa ilivyo nchini. Kulia ni Afisa Mafunzo
wa TMF, Raziah Mawanga, Mwenyekiti wa MISATAN, Simon Berege na Ofisa
Miradi katika Kitengo cha Mawasiliano na Tehama UNESCO, Nancy Kaizelege.

Afisa
Mafunzo wa TMF, Raziah Mawanga akizungumza jinsi TMF inawasaidia
waandishi wa habari ili waweze kufanya kazi zao kwa weledi. Kushoto ni
Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Jamhuri na Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la
Wahariri (TEF), Deodatus Balile. Kulia ni Mwenyekiti wa MISATAN, Simon
Berege na Ofisa Miradi katika Kitengo cha Mawasiliano na Tehama UNESCO,
Nancy Kaizelege.

Ofisa
Miradi katika Kitengo cha Mawasiliano na Tehama UNESCO, Nancy Kaizelege
akizungumzia ushiriki wa UNESCO katika kuandaa Siku ya Uhuru wa Vyombo
vya Habari ambapo kwa mwaka huu zinafanyika Mwanza. Kushoto ni
Mwenyekiti wa MISATAN, Simon Berege na Afisa Mafunzo wa TMF, Raziah
Mawanga.

Afisa
Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia
Nkhoma-Ledama akieleza kazi za Umoja wa Mataifa ili kuvisaidia vyombo
vya habari kupata uhuru wa kufanya kazi bila kuingiliwa.

Post a Comment