MTANGAZAJI

WAZIRI NCHEMBA AKUTANA NA RAIS WA VIETNAM

Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi  Mh.Mwigulu Lameck Nchemba amefanya mazungumzo na Rais wa Vietnam mapema hii leo.

Katika mazungumzo yao,Mwigulu anasema "Ni kweli leo nimekuwa na mazungumzo na Rais wa Vietnam kuhusu sekta ya kilimo,mifugo na uvuvi.

Katika mazungumzo hayo wameangalia namna gani Tanzania  itaongeza uzalishaji wa mbegu bora za mazao na uzalishaji wa samaki ilikupambana na uvuvi usio na tija,Uhitaji mkubwa wa masoko ikiwemo uzalishaji wa mafuta ya kula kwa kiwango cha kutosha hapa nchini.

Pia viongozi hao wamezungumzia swala la uzalishaji wa sukari na mpunga wa kutosha hapa hapa nchini.

Waziri Nchemba ameeleza kuwa wanakwenda kutumia fursa hii kupitia balozi za Tanzania kwa wafanyabiashara wa nchi hizi mbili kupeana taarifa za kibiashara na uwekezaji hapa nchini ilikupanua wigo wa kukua kwa uchumi wetu.
Picha na Festo sanga Jr.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.