TAARIFA ZA UONGO KUHUSU RAIS MAGUFULI KUZURU NCHINI KENYA
Kumekuwepo na habari za uongo na potofu katika mtandao wa jamii wa www.kenya-today.com
kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph
Magufuli atazuru Kenya kuhudhuria kumbukumbu ya marehemu Mhe. Jaramongi
Odinda na Fidel Odinga Jumamosi hii.
Inasikitisha
kuona kwamba mwandishi wa Kenya anachukua nafasi ya Mwanahabari wa Rais
wa Tanzania kwa kuwa na ratiba ya Mhe. Rais wa Tanzania kuliko
waTanzania wenyewe.
Haijulikani
ni nini has nia ya mtandao huo, lakini ukweli ni kwamba ratiba hiyo ni
batili na ya uongo uliotukuka. Hawa watani wetu wa jadi wana lao jambo!
Wapuuzeni. Taarifa hiyo si ya kweli.
Chanzo:Issa Michuzi
Post a Comment