MOROGORO:UJUMBE KIONGOZI WA KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO DUNIANI BAADA YA KUSHIRIKI ZOEZI LA USAFI NCHINI TANZANIA LE
Makamu wa Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Wasabato Duniani Mchungaji Geofrey Gabriel Mbwana (pichani) yuko nchini Tanzania na hii leo ameshuhudia na kushirikia zoezi la usafi nchi nzima kwa mara ya kwanza ambalo limeandana na kusherekea siku ya uhuru.
Mchungaji Mbwana ambaye ni mtanzania yuko nchini kwa likizo yake ya mwisho wa mwaka ameandika katika wasifu wake wa facebook maneno haya;
NIMESHUDIA KWA MACHO NA KUSHIRIKI:
Asubuhi ya leo Desemba 9,2015 nimesherehekea uhuru wa nchi yangu kwa KUSHIRIKI mwito wa Rais Magufuli kwa kufanya usafi. Sherehe imenikuta nikiwa nyumbani kwa mama mzazi mjini Morogoro, Mtaa wa Vibandani. Mapema asubuhi sana nilisikia mifagio, majembe, mafyekeo, nk vikifanya kazi.
Hata niandikapo bado nasikia sauti ya vitendea kazi hivyo vikifanya kazi - Ni kama muziki wa sauti za ndege asubuhi kunapokucha. Nilipotoka nikaona Watanzania wenzangu wakifanya kazi za usafi kwa furaha wakibadilishana busara chache hapa na pale wakionyesha walivyofurahishwa na agilizo la Raisi wetu.
Ilinivutia sana na hisia za kujivunia nchi yangu zikanijaa. Nikajisikia nikijiambia mwenyewe: "Kwa namna hii TZ na Watanzania tunakuwa kielelezo na kivutio kikubwa ulimwenguni.
Kwa namna hii bili ya taifa ya TIBA itapungua na fedha hizo, kwa namna ya usimamizi anaouonyesha Raisi Magufuli, zitaelekea kwenye shughuli muhimu za kuboresha maisha yetu Watanzania.
' Sikuishia kushuhudia na kutamka hayo Bali nilikwenda mara nikachukua mfagio na reki nami nikaungana na Watanzania wenzangu kufanya usafi tena kwa furaha tele nikimuunga mkomo Raisi wa nchi yangu Tanzania.
Mwandishi mmoja nashukuru alisema:
USAFI NA UWE MTINDO WA MAISHA. NAJIVUNIA TANZANIA SAFI NA WATANZANIA NADHIFU.
USAFI NA UWE MTINDO WA MAISHA. NAJIVUNIA TANZANIA SAFI NA WATANZANIA NADHIFU.
Post a Comment