MTANGAZAJI

SITOKUWA TAYARI KUTOA MATUMAINI HEWA KWA WANANCHI AMBAYO HAYATEKELEZEKI-DKT MAGUFULI
  Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Ifakara wilayani Kilombero kwenye mkutano wa kampeni za CCM ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa wakati wake utakuwa wa kiutendaji zaidi ili kufanikisha maendeleo ya haraka kwa nchi na wananchi kwa jumla.

Picha na Michuzi Jr-Kilombero.

  Wananchi wa mji wa Ifakara waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni za CCM ndani ya uwanja wa saba saba wilayani Kilombero,wakimshangilia kwa shangwe Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipowahutubia kwenye mkutano huo.
  Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimtambulisha mgombea ubunge jimbo la ilombero Ndugu Abubakar Assenga almaarufu kama mtoto wa fundi Cherehani kwenye mkutano wa kampeni za CCM zilizofanyika Ifakara wilayani Kilombero.

Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Ifakara wilayani Kilombero kwenye mkutano wa kampeni za CCM.

Mgombea  urais kwa tiketi ya CCM, Dk.John Magufuli amesema  kuwa katika kipindi hiki cha kuomba ridhaa ya wananchi ili awe Rais hatakuwa tayari kutoa matumani hewa ambayo anajua wazi hayatekelezeki kwani ni dhambi na kufafafanua kila anachoahidi anauhakika anao uwezo wa kutekeleza.

 Dk.Magufuli aliwambia wananchi wa Ulanga kuwa anatambua dhamana anayoomba kwa wananchi lakini ana uhakika malengo yake ya kuwatumikia Watanzania na kuleta maendeleo yatafanikiwa kwani iwapo atahitaji ushaauri ataupata kwa viongozi waliomtangulia kuongoza nchi.

Alisema kiongozi mzuri ni Yule ambaye anaweka malengo ya kuwatumikia wananchi kwa misingi ya uzalendo na uadilifu na anapoona kuna mambo yanahitaji ushauri kabla ya kufikia uamuzi wapo viongozi wa kumshauri na kumpa mbinu za kufanya.

Dk.Magufuli ameanza awamu ya pili ya kampeni baada ya kumaliza mikoa ya Nyanda za Juu Kusini na Mkoa mmoja wa Kusini wa Mtwara ambapo jana ameanza ziara Mkoa wa Morogoro.

 Msafara wa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi,Dkt John Pombe Magufuli  ukikatiza kwenye dara la muda la Mto Kilombero,ambalo hutumika kupitishia vifaa mbalimbali kwa ajili ya ujenze wa daraja kubwa linalojengwa katika mto huo wa kilombero.
 Dkt John Pombe Magufuli  akikagua daraja la Mto Kilombero ambalo ujenzi wake unaendelea mpaka sasa. 


 Baadhi ya Viongozi wa Dini wakimwombea sala  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi,Dkt John Pombe Magufuli  mara baada ya kumaliza kuhutubia  jioni ya leo kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi Mahenge jioni ya jana.
 
 Mkutano wa kampeni za CCM ulipokuwa ukiendelea katika uwanja wa saba saba mjini Ifakara wilayani Kilombero jioni ya leo.
 Mfuasi wa CCM na bango lake
  Wananchi wa mji wa Ifakara waliojitokeza kwenye mkutano wa kampeni za CCM ndani ya uwanja wa saba saba wilayani Kilombero,wakimsikiliza kwa makini mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipowahutubia kwenye mkutano huo.
  Mgombea ubunge jimbo la ilombero Ndugu Abubakar Assenga almaarufu kama mtoto wa fundi Cherehani akizungumza jambo kwenye mkutano wa kampeni za CCM zilizofanyika Ifakara wilayani Kilombero jioni ya leo.
 Wananchi wa mji wa Ifakara walaiojitokeza kwa kwenye mkutano wa kampeni za CCM ndani ya uwanja wa saba saba wilayani Kilombero,wakimsikiliza kwa makini mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipowahutubia kwenye mkutano huo. 
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi,Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi Ilani ya CCM Mgombea Udiwani wa CCM wilaya ya Ulanga jioni ya leo kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya msinfi Mahenge jioni ya leo.
 Wananchi wakifuatilia hotuba ya Magufuli alipokuwa akipita kuwasalimia wananchi wa kijiji cha Lupiro-Ifakara wilayani Kilombero
Wananchi wa kijiji cha Lupiro-Ifakara wilayani Kilombero wakiwa wamefunga bara bara wakimsimamisha Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi,Dkt John Pombe Magufuli  awasalimie alipokuwa akitokea Malinyi

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.