MTANGAZAJI

SERIKALI:WANAFUNZI NA WATU WENYE ULEMAVU KUSAFIRI BURE KATIKA KIVUKO CHA MV MAFANIKIO CHA MTWARA
Sehemu kivuko kilichozinduliwa juzi na Rais Dkt Jakaya Kikwete huko Mtwara


 
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiknjxuv_xRPWLIc48GBf9Y2IiiFp7o7j_02VBm0iJu2BJQMZ5SDanCX91Hcx00iSbpOsGEuauCkGa8fFhUtHQj_zFGL_aWPctY7AAwWcwQBDAEp3cCKQJ0NfwgIcsE1g1UOFBwoqeUJHUc/s1600/_MG_4226.jpg

 Rais Kikwete akizindua rasmi kivuko cha MV Mafanikio kwenye pwani ya mji wa
Mtwara kitachofanya safari kutokea Msemo kuelekea Msangamkuu
Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais Jakaya
Kikwete kabla ya uzinduzi wa kivuko cha Mv Mafanikio mkoani Mtwara ,kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mh.Fatma Salum Ali

Waziri wa Fedha Mh.Mwigulu Nchemba akiteta jambo na Waziri wa Ujenzi
Mh.John Pombe Magufuli kabla ya uzinduzi wa Kivuko cha Mv Mafanikio
mkoani Mtwara (Picha zote na Michuzi Jr)Serikali ya Tanzania imeagiza wanafunzi na watu wenye ulemavu katika Manispaa ya Mtwara Mikindani na kata ya Msangamkuu, watasafiri bure kwenye kivuko cha Mv Mafanikio.

Kauli hiyo ilitolewa juzi na Waziri wa Ujenzi, John Magufuli,  wakati akimkaribisha Rais Jakaya Kikwete kuzindua kivuko hicho.

Amesema walemavu na wanafunzi wote waliovaa sare za shule hawatatozwa nauli kutokana na kundi hilo kuwa tegemezi.
  
Magufuli amesema kivuko hicho chenye uwezo wa kubeba abiria 100 pamoja na magari kimegharimu Sh. milioni 3.3, fedha kutoka serikalini. 

Akihutubia wananchi wa Msangamkuu pamoja na Mtwara wakati wa uzinduzi huo,  Rais Jakaya Kikwete amesema serikali imetatua kero hiyo ya kivuko iliyokuwa ikiwakabili wananchi kwa muda mrefu.
 
Amesema  kutokana na wakazi wa maeneo hayo kukosa kivuko tangu kupatikana kwa uhuru, watu wengi walipoteza maisha na kuwataka kukitumia kivuko hicho  vizuri.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.