MTANGAZAJI

MWANZA:BILIONI MOJA NA NUSU ZATUMIKA KUJENGA HOSPITAL YA WAADVENTISTA WA SABATO YA MWANZA (MAMC)

Hospitali ya Waadventista Wa Sabato ya Mwanza (MAMC) inavyoonekana kwa sasa.


  Hospitali ya Waadventista wa Sabato, Mwanza Adventist Medical Centre(MAMC),sasa iko katika hatua za mwisho za Ujenzi.


Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afya ya Kanisa la Waadventista wa Sabato Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania (NTUC), Dk Silas Kabhele, amesema zaidi ya shilingi bilioni moja na nusu za Tanzania  zimetumika kujenga Hospitali hiyo.

 Dk.Kabhele ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Afya katika Jimbo la Kusini  mwa Ziwa Nyanza(SNC) amesema hivi karibuni  kwamba sasa zinahitajika takriban shilingi milioni 600 kukamilisha ujenzi.

Hospitali hiyo ya Gorofa tano tayari paa limeezekwa,kuta zote za nje zimepigwa lipu na kwamba hata baadhi ya kuta za ndani zimepigwa lipu.



Hospitali ya Pasiansi ikikamilika itafanana hivi


No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.