DAR ES SALAAM:SERIKALI, UN NA VYOMBO VYA HABARI KUTOA ELIMU DHIDI YA EBOLA
Mkurugenzi
Msaidizi Kitengo cha Elimu ya Afya kwa Umma kutoka Wizara ya Afya na
Ustawi ya Jamii, Said Makora (kulia), akielezea jinsi Wizara hiyo
inavyopambana kutoa elimu ya ugonjwa wa Ebola kwa wananchi wakati wa
kongamano lililoandaliwa na UNESCO, WHO, UNICEF, Wizara ya Afya na
Ustawi ya Jamii, uliofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu Huria cha
Tanzania (OUT), Novemba 11,2014 jijini Dar es Salaam mkutano huo
uliowakutanisha wamiliki wa Redio za kijamii kuwaelimsha Radio za
Kijamii za Mikoani ni namna gani wanavyoweza kushirikiana na Wizara ya
Afya na Ustawi ya jamii ili kutoa taarifa sahihi kwa wananchi kuhusu
ugonjwa wa Ebola, Ebola ni nini namna ya kujinga na dalili
zake.(kushoto), Kushoto ni Mwenyekiti wa COMNETA ambaye pia ni
Mkurugenzi wa Redio FADECO, Sekiku Joseph.(PICHA NA PHILEMON SOLOMON).
Na Mwandishi wetu
SERIKALI
, Mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN) na vyombo vya habari nchini hapa
vimekubaliana kufanyakazi kwa pamoja kwa ajili ya kuelimisha watanzania
kuhusu ugonjwa hatari wa Ebola.
Katika
juhudi za kuwekana sawa kuhusu uelimishaji wa umma kuhusu ugonjwa huo,
kumefanyika kongamano la mafunzo kwa siku mbili, Chuo Kikuu huria jijini
Dar es salaam.Kongamano hilo lilifanyika Novemba 10 na 11.
Kongamano hilo liliwashirikisha viongozi wa radio za wananchi zaidi ya 28 kutoka Visiwani na Tanzania Bara.
Katika
kongmano hilo kulitengenezwa mikakati mbalimbali yenye kuleta uelewa
kwa umma na kuwafanya kuchukua hatua za tahadhari na kuzuia ugonjwa huo
usiingie nchini.
Mshauri
wa Redio Jamii na Mkufunzi kutoka Shirika la Kimataifa la Elimu Sayansi
na Utamaduni (UNESCO) Bi. Rose Mwalimu akiendesha majadiliano kuhusu
mikakati endelevu itakayowezesha kuihusisha jamii katika upatikanaji wa
taarifa sahihi juu ya ugonjwa wa Ebola wakati wa kongamano hilo
lililowakutanisha wamiliki wa radio za kijamii lengo ni kuwaelimsha
Radio za Kijamii za Mikoani ili kutoa taarifa zilizo sahihi kwa wananchi
kuhusu ugonjwa wa Ebola.
Kwa
mujibu wa mmoja wa watu wanaounda kikundi kazi chenye lengo la
kukabiliana na ugonjwa huo mafunzo hayo yaliandaliwa na Shirika la
sayansi, elimu na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) .
Aidha
mafunzo hayo yaliwezeshwa kwa pamoja kati ya wizara ya afya na Umoja wa
Afya duniani (WHO), na Shirika la kusaidia watoto la UNICEF.
Mafunzo
hayo yaliyokuwa na washiriki walikuwa ni pamoja na wanachama wa
wanamtandao wa vyombo vya habari Tanzania (COMNETA), yaligusa zaidi
redio ambapo 25 kati yake zinaohudumiwa na Umoja wa Mataifa.
Wakati
lengo kuu ni kuwafanya watanzania waujue ugonjwa huo na kuanza kuchukua
hatua za tahadhari, mafunzo yalilenga kushawishi vyombo hivyo kutenga
muda mchache kwa ajili ya elimu hiyo ili kuzuia mlipuko wake nchini.
Mkurugenzi
wa Redio Kwizera ilioko Ngara-Kagera, Damas Missanga akichangia mada
yake wakati wa kongamano la kuwaelimsha wamiliki wa Redio za Kijamii za
Mikoani ili kutoa taarifa zilizo sahihi kwa wananchi kuhusu ugonjwa wa
Ebola.
Katika
mafunzo hayo washiriki walidadavua ebola nini na jamii inaweza
kujijenga namna gani ili kukabiliana na janga hilo la kidunia.
Matumizi
ya elimu ya mawasiliano yalitiliwa mkazo hasa kwa kubaini kwamba elimu
hiyo ndiyo itakayoweza kutengeneza mkakati wa kuwabadili wengine na
hivyo kuzuia kuingia kwake na kusambaa.
Washiriki
na wawezeshaji walikubali kufanyakazi ya pamoja na Tume ya taifa
inayoratibu mapambano dhidi ya Ebola katika kuelimisha umma kwa kuweka
wazi taarifa za ugonjwa huo na namna ya kukabiliana nao.
Ilikubaliwa
kwamba radio hizo za jamii zitatumika kuanzisha midahalo yenye lengo la
kuwasilisha taarifa mbalimbali kutoka kwa kikosi kazi cha kukabiliana
na ugonjwa huo.
Meneja wa Redio jamii FADECO ya wilayani Karagwe, Adelina Lweramula akichangia mada wakati wa kongamani hilo.
Wamiliki
wa Redio za Kijamii wakiwa katika mkutano ulioandaliwa na UNESCO, WHO,
UNICEF, Wizara ya Afya na Ustawi ya Jamii ili kuwaelimsha wa wamiliki
hao kutoa taarifa zilizo sahihi kwa wananchi kuhusu ugonjwa wa Ebola.
Post a Comment