MTANGAZAJI

MGANGA WA KIENYEJI AHUKUMIWA MIAKA 30 JELA KWA KOSA LA UBAKAJI

Mganga wa kienyeji amehukumiwa miaka 30 jela baada ya mahakama ya Wilaya ya Tarime kumkuta na kosa la kubaka binti wa miaka 13 (jina limehifadhiwa) katika kijiji cha Panyakoo Wilayani Rorya mapema mwezi januari mwaka huu. 

Sangoma huyo aliyetambuliwa kwa jina la Joseph Marando Ikanda (53) mkazi wa kijiji cha Raranya  alitenda kosa hilo Januari 19, 2014 majira ya 10 jioni nyumbani kwao na binti huyo katika kijiji cha Panyakoo alikokuwa ameenda kufanya kazi ya kumtibu baba mdogo wa binti huyo.

Akisoma hukumu hiyo hakimu mfawidhi wa mahakama ya Wilaya ya Tarime Adrian Kilimi amesema kuwa Joseph alikuwa ameishi hapo  kwa muda wa miezi mitatu akifanya shughuli ya uganga hivyo haikuwa vigumu kumshawishi mtoto huyo kufanya kitendo hicho kichafu.


Amesema kuwa siku ya tukio Ikanda alimwagiza binti huyo sigara kwa kumpa kiasi cha pesa, lakini sigara aliikosa na binti  kumrudishia pesa  hapo alimshawishi kuwa  binti huyo anaonekana kuwa na tatizo hivyo alihitaji kumpa dawa ,na kwa kuwa binti huyo alikuwa akiona wenzake wakipewa dawa alikubali na kumruhusu mganga aendelee.

Mwendesha mashitaka wa  serikali Inspector George Lutonja ameiambia mahakama kuwa baada ya kumaliza ufedhuli huo mtoto  alitoka nje akilia kutokana na maumivu, watu waliokuwa nje wakisubiri kupata huduma walimuulizia kujua kilichokuwa kimetokea ambapo binti aliwaliwasimulia kisa kizima.


Wananchi  hao walimkamata mganga huyo na kumpeleka kituo cha polisi Panyakoo huku binti huyo akipelekwa kituo cha afya Rorya kupata matibabu.

Mtuhumiwa  alifikishwa kituoni na kufunguliwa jalada kisha januari 22,alifikishwa mahakamani kusomewa shauri lake huku akiendelea kusota rumande hadi Agosti 7, 2014 hukumu ilipotolewa dhidi yake.


Akisoma hukumu hiyo Hakimu mfawidhi wa mahakama ya Wilaya Adrian Kilimi amesema  baada ya kusikiliza pende zote mbili za mlalamikiwa na mlalamikaji na kuleta mashahidi, mahakama imemkuta mlalamikiwa na kosa la kubaka na kuhukumiwa miaka 30 jela.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.