MTANGAZAJI

DAR ES SALAAM:SERIKALI YAWATAKA WAIMBAJI WA KWAYA ZA WAADVENTISTA WASABATO KUSAJILI NYIMBO ZAO BARAZA LA SANAA LA TAIFA
Naibu Waziri wa Sheria na Katiba Angellah Kairuki akihutumia katika uzinduzi huo


 

 

Naibu Waziri wa sheria na katiba Anjela Kairuki amezitaka kwaya za makanisa ya Waadiventista Wa Sabato nchini Tanzania  kusajili matoleo ya nyimbo wanazoimba kwa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ili kupata fursa mbalimbali kutoka serikalini.

Agizo hilo amelitoa hapo jana katika uzinduzi wa toleo la sita la video ya waimbaji wa kwaya ya Kanisa la Waadivestista Wa Sabato Kurasini inayoitwa Tufundishe Kuabudu uliofanyika katika viwanja vya maonesho ya sabasaba jijini Dar-es-saalam.

Angellah Kairuki amesema kuwa kwaya zinapaswa kusajili nyimbo zake basata ili kuweza kunufaika kiuchumi kutoka katika mamlaka mbalimbali za serikali ikiwemo zinazowezesha wananchi kiuchumi.

Amesema serikali itaendelea kuwasaidia wasanii mbalimbali zikiwemo kwaya katika kupata miundo mbinu mbalimbali ili kuweza kufanya kazi kwa ufanisi na hilo litafanyika iwapo kwaya hizo zitakuwa zinatambuliwa kupitia BASATA na Wizara ya Habari,Vijana Utamaduni na Michezo.

Uzinduzi huo ulioshuhudiwa na mamia ya wakazi wa jiji na Dar es salaam  uliwakutanisha waimbaji wa Mbiu kwaya,Mburahati,Nyegezi,light beares,Royal Advent ,Vocapella,KKKT Keko,Namsifu Mbuso na Masalio Echoes toka Nairobi nchini Kenya.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.