TABORA:WAALIMU WAAGIZWA KUFUATILIA MAHUDHURIO YA WATOTO SHULENI
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Sikonge mkoani
Tabora Robert Kamoga amewaagizi waalimu
wakuu wa shule zote za msingi katika wilaya hiyo kuhakikisha wanafuatilia mahudhurio ya watoto
shuleni,ili kubaini watoto wasiofika shuleni
ili wazazi wao wakamatwe mara
moja na kutozwa faini.
Kamoga
ametoa agizo hilo alipokuwa akizungumza na mamia ya wananchi waliojitokeza
katika maadhimisho ya siku ya kupinga utumikishwaji kwa watoto iliyofanyika kimkoa katika kijiji
cha Udongo kata ya Ipole wilayani Sikonge mkoani Tabora.
Sambamba na
hilo amewaagiza watendaji wote wa halmashauri hiyo kuanzia ngazi ya vijiji na
kata kuwachukulia hatua kali watu wote watakaobainika kujihusisha na vitendo
vya utumikishwaji watoto katika maeneo yao .
Kamoga amepongeza jitihada zinazofanywa na mradi wa
PROSPER katika kutokomeza utumikishwaji watoto kwenye shughuli za kilimo katika
wilaya hiyo.
Tabora ni miongoni
mwa mikoa 5 inayoelezwa kuwa inaongoza kwa umaskini hapa nchini na asilimia kubwa
ya wananchi wake ni maskini hali inayochangia watoto wengi kutumikishwa katika
kazi ngumu kwa ujira mdogo.
Sheria ya mtoto na.21 ya mwaka 2009 kifungu cha 78 (1)
inakataza mtu yeyote kuajiri au kutumikisha watoto katika shughuli
yoyote ile inayowaathiri watoto.
Post a Comment