MTANGAZAJI

SITA WAHOFIWA KUFA MAJI KATIKA ZIWA VICTORIA

Watu sita kati ya 11 waliokuwa wakisafiri kwa kutumia boti wanahofiwa kufa maji huku watano wakiwa wameokolewa na wengine hawajulikani walipo baada ya boti hiyo kuzama hapo jana katika Ziwa Victoria.

Mwili wa mtu mmoja alitambuliwa kwa jina la Jehn Mwulyatete raia wa Rwanda umepatikana ukielea baada ya kuwa unasukumwa na mawimbi.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera ,George Mayunga amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kwamba ajali hiyo ilitokea eneo la Bugombe katika kisiwa cha Kasenyi Muganza wilaya ya Chato mkoani Geita.

Mafunga ameeleza kuwa chanzo cha hiyo ni upepo mkali uliotokea jana Ziwa Victoria majira ya usiku na kusababisha mendeshaji wa boti hiyo kushindwa kuimudu kutokana na shehena kubwa ya dagaa zilizokuwa ndani yake.


No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.