MWANAMKE MJAMZITO HUKO SUDAN AHUKUMIWA KUNYONGWA BAADA YA KUBADILI DINI NA KUWA MKRISTO
Mahakama ya
Sudan imemhukumu mwanamke mjamzito adhabu ya kunyongwa baada ya kubadili dini
na kuwa mkristo.
Tovuti ya
shirika la habari la Sky News hii leo imemtaja mwanamke huyo kuwa ni Mariam Yahya(27)
ambaye alikamatwa pamoja na mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miezi 20 na
aliamuliwa kuikana Imani yake na kurudi katika dini ya kiislamu.
Pia
ameshitakiwa kwa kosa la kuolewa na mwanamme mkristo.
Adhabu hiyo
ya kifo ilitolewa japo kuwa barozi za mataifa ya magharibi ziliomba uhuru wa
kuabudu uheshimiwe.
Katika
Mahakama ya Khartoum Jaji Abbas Al Khalifa alisema “Tulikupa siku tatu za
kuacha uamuzi wako lakini ukasisitiza kutorudi katika uislamu,ninakuhukumu
kunyongwa”
Mwanamke
huyo aliyezaliwa na mwanamke mwislamu alihukumiwa katika sharia za kiislamu
ambayo ilipitishwa kwa lazima nchini Sudan mwaka 1983.
Mariam Yahya
ameolewa na mkristo raia wa Sudani ya Kusini ambayo ilipata uhuru wake mwaka
2011 baada ya vita vya wenyewe.
Kabla ya
hukumu hiyo viongozi wa dini ya kiislamu walizungumza na mwanamke huyo kwa muda
wa dakika 30 wakimshawishi kurudi katika Imani yake ya kwanza na alimwambia
jaji kuwa yeye ni mkristo.
Kufuatia
adhabu hiyo mmoja wa wanasheria wake Mohanad Mustafa amesema atatafuta njia ya
kukata rufaa kuhusu hukumu hiyo.
Jumla ya
watu 100 miongoni mwao wakiwa ni wawakilishi wa barozi mbalimbali za mataifa ya
magharibi ambayo ni Marekani,Canada na Uholanzi walihudhuria mahakamani hapo.
Post a Comment