MELI ILIYOKUWA NA ABIRIA 460 YAZAMA KATIKA PWANI YA KOREA YA KUSINI
Oparesheni
ya uokozi inaendelea kufuatia ishara za dharura zilizoripotiwa kutokana na meli moja iliyobeba takriban abiria 460 katika
pwani ya Korea Kusini kuzama.
Maafisa
wanasema kuwa walinzi wa pwani hiyo wanatumia, meli za wanamaji wa Korea pamoja
na ndege za uokoaji kuwaokoa watu waliokuwa katika meli hiyo.ambapo abiria 160 wameokolewa
na wengine wakishauriwa kuruka baharini ili waokolewe.
Meli hiyo
ilikuwa imebeba idadi kubwa ya wanafunzi ikitoka Incheon iliyoko kwenye visiwa
vya kifahari vya Jeju .
Shughuli
ya uokoaji bado inaendelea na walioshuhudia ajali wanasema kulisikika kishindo
kikubwa kabla ya ferry hiyo kuanza kuzama zaidi ya kilomita 20 kutoka ufukweni.
Chanzo:BBC
Post a Comment