WAKAZI WA TABATA DAR ES SALAAM WAKERWA NA TANESCO KUTOWAPATIA UMEME
Wakazi
wa Tabata Kisiwani jijini Dar-es-saalam wamekerwa na kitendo cha kuachwa na
shirika la ugawaji wa umeme nchini Tanesco katika hali ya wasiwasi na giza kila uingiapo usiku kwa zaidi ya wiki moja sasa baada ya Tanesco kukata umeme katika
eneo hilo .
Kutokana
na nguzo ya umeme kuangukia moja ya nyumba na nyaya zake kushuka chini kiasi
cha kuchezewa na watoto huku wakidai
kuwa shirika hilo halijarejea kuresha huduma hiyo .
Edward
Luoga ambaye ni mkazi wa eneo hilo anasema kuwa matatizo haya yametokana na
mvua kubwa zinazoendelea kunyesha chini kwa
wingi khali inayosababbisha uharibifu wa miundombinu hiyo.
Amesema
nguzo iliyoanguka katika maeneo hayo ni
miongoni mwa vyanzo vya matatizo ya nishati hiyo ya umeme
katika eneo hilo.
Wakazi
hao wamesema tangu shirika hilo lifike katika eneo la tukio na kuona yaliyojiri
lilikata huduma hiyo na hivyo kupelekea changamoto kubwa ya huduma hiyo kwa
maeneo hayo jijini.
Post a Comment