MTANGAZAJI

WAADVENTISTA WA SABATO WATAKIWA KUTUMIA VYOMBO VYA HABARI VYA KANISA HILO

Wito umetolewa kwa waumini wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato nchini Tanzania kuona umuhimu wa matumizi ya vyombo vya habari vya kanisa kwa ajili ya kazi ya uinjilisti .

Akizungumza mapema hii leo mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere,Mwenyekiti wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato toka nchi za ukanda wa Afrika mashariki na kati mchungaji Blusious Ruguri amesema kuwa wakati umefika sasa kwa kanisa kwa ujumla kuhubiri injili kwa kutumia vyombo vya habari mbali na njia ile ya zamani yakutumia mikutano ya adhara.


Akizungumzia maandalizi ya urushwaji wa matangazo ya morning star Televisheni Mchungaji Ruguri ameongeza kuwa uanzishwaji wa matangazo ya kituo hiki kipya kitaongeza kasi ya ukuaji wa makanisa na kazi ya uinjilisti kwa ujumla pia amekipongeza kituo cha radio ya Morning Star kutokana na mchango wake mkubwa katika kutangaza injili ya marejeo ya Kristo.


Mch Ruguri pamoja na viongozi mbalimbali wa ngazi zajuu za kanisa la waadiventista wasabato wako hapa nchini kwa ajili ya kushuhudia sherehe za maandalizi ya urushwaji wa matangazo ya kituo kipya cha kanisa cha morning star Televisheni Apr 19 mwaka huu katika viwanja vya PTA.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.