MTANGAZAJI

UTAFITI:WANANCHI WACHACHE WA WILAYA TATU ZA MKOA WA DODOMA WANATUMIA VYOO BORA

Utafiti uliofanywa kwenye wilaya za Bahi,Chamwino na Kongwa mkoani Dodoma umebaini asilimia 27 tu ya wananchi ndio wanaotumia vyoo bora huku asilimia tatu pekee ndio hunawa mikono wanapotoka chooni.

Mtafiti Johnstone Andrea ametoa taarifa ya utafiti huo jana wakati wa tathimini ya Mradi wa Usafi wa Mazingira Tanzania (UMATA) unaotekelezwa katika wilaya tatu za mkoa wa Dodoma.


Utafiti huo umefanyika ili kuona utekelezaji wa mambo yaliyokusudiwa kuboresha hali ya wananchi katika wilaya hizo tatu ambazo zilikuwa uhitaji mkubwa kutokana na hali ya usafi wa mazingira na vyoo kuwa chini sana.


Utafiti huo ulibaini kuwa asilimia 53 hadi 54 ya wananchi walikuwa na uwezo wa kupata maji safi kupata maji safi na salama licha ya kuwa na changamoto ya umbali kutoka nyumbani hadi maji yanapopatikana.


Mganga mkuu wa wilaya ya Chamwino James Charles anasema asilimia 40 hadi 60 ya magonjwa husababishwa na uchafu na kutopatikana kwa maji safi na salama.


Chanzo:Gazeti la Habari Leo

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.