MTANGAZAJI

MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA YATOA TAHADHARI KUHUSU MVUA KUBWA

Tahadhari imetolewa na Mamlaka ya hali ya Hewa Tanzania (TMA) ya mvua kubwa kunyesha kuanzia leo na kesho katika ukanda wa Pwani.

Katika taarifa yake kwa umma jana jioni TMA imesema maeneo ambayo yataathiriwa na mvua hizo za kuanzia leo ni visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na mikoa ya Tanga,Pwani na Dar es salaam.


Huu ni mwendelezo wa mvua zilizosababisha maafa makubwa ambazo zilianza kunyesaha april 10 mwaka huu katika ukanda huo mwa Pwani,maeneo yaliyokuwa yameathiriwa zaidi ni Dar es salaam na Morogoro ambako zaidi ya watu 25 wallifariki dunia.


Mbali ya vifo hivyo mvua hizo zilisababisha uharibifu mkubwa wa miundo mbinu ya barabara hasa madaraja,ambapo Mawasiliano ya Barabara kati ya mkoa wa Dar es salaam na mingine nchini yalikatika kwa siku mbili baada ya barabara zake zote zinazounganishwa na maeneo hayo ama kuharibiwa vibaya na mafuriko au kujaa maji na kushindwa kupitika.


Taarifa hiyo ya TMA imesema mvua hizo zinatarajiwa kuwa kubwa kwani zitazidi milimilita 50 katika saa 24 ,wakazi wa maeno hatari,watumiaji wa bahari pamoja na mamlaka zinazohusika na maafa wanashauriwa kuchukua tahadhari stahiki ilisema taarifa hiyo.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.