BIASHARA YA NGONO,KUJAMIANA KINYUME NA MAUMBILE VIKWAZO KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI
Kushamiri kwa biashara ya ngono katika maeneno ya
mijini,tabia ya kujamiana kinyume na maumbile na matumizi ya dawa ya kulevya
imetajwa kuwa ni vikwazo vikubwa katika mapambano dhidi ya UKIMWI.
Licha ya kasi ya maambuzi ya virusi vya ugonjwa huo kupungua kutoka
asilimia saba mwaka 2003 hadi asilimia 5.1 mwishoni mwa mwaka juzi lakini takwimu za kitaifa zinaonesha kuwa kwa
watu walioko katika makundi hayo maambukizi yamefikia hadi asilimia 40.
Taarifa hiyo imetolewa katika washa ya siku mbili iliyoendeshwa na tume
ya taifa ya kudhibiti UKIMWI nchini Tanzania (TACAIDS) kwa ajili ya kusambaza
mkakati wa tatu kwa wadau mbalimbali kutoka katika mikoa ya Tabora Shinyanga,Simiyu
na wenyeji Singida.
Pamoja na mambo mengine yaliyoanishwa katika mkakati
huo,msisitizo mkubwa wa Maofisa wa TACAIDS kwa halmashauri nchini kuelekeza nguvu zao
kwa makundi maalum.
Mapendekezo ya wadau katika kukabiliana na tatizo ni
kurekebisha sheria zilizopo na kutoa elimu zaidi kwa jamii.
Usambazaji wa mkakati wa tatu wa Taifa kwa ajili ya
kudhibiti Ukimwi nchini Tanzania ,unalenga kupunguza kasi ya maambukizi ya
ugonjwa huo hadi kufikia asilimia 0.16 ifikapo mwaka 2018.
Post a Comment