MTANGAZAJI

ASHIKILIWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA KUTAKA KUMUUA MWANAYE

Jeshi la polisi mkoani Simiyu linamshikilia mkazi mmoja wa kijiji cha Songambele wilaya ya Maswa mkoani Simiyu kwa tuhuma za kutaka kumuua mtoto wake kwa kumtupa na kumtelekeza nje ya nyumba ili aliwe na fisi.

Kamanda wa polisi mkoani Simiyu ,Bwana Charles Mkumbo amesema kuwa tukio hilo limetokea mapema wiki hii saa nane za usiku wakati mtuhumiwa Bwana ,Baya Seni akiwa amelala ana familia yake kijijini hapo ,ndipo alikurupuka ndani na kumpiga mtoto wake na kisha kumtupa nje kwa lengo la kumteleza nje ya nyumba.


Bwana Mkumbo aliongeza kuwa mtuhumiwa alifanya hivyo kwa kuwa hakuona thamani ya mtoto wa kiume kwenye familia yake kwani uzoefu unaonya watoto wa kiume wakikua hudai kupata mirathi kutoka kwa wazazi wao,ikilinganishwa na watoto wa kike kwani wanapoolewa uleta mifugo na pesa kama mahari na pia siyo mizigo kwa wazazi kwani uhamia kwenye familia atakayo olewa.


Kwa upande wake mama wa mtoto huyo Bi Elizabeth Paulo amesema ,mume wake alikuwa akimtesa sana mtoto wake akimbagua kwa vile yeye ni wa jinsia ya kiume na hana faida kwake.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.