IDADI YA WAGONJWA WA KIFUA KIKUU JIJINI ARUSHA YAONGEZEKA
Idadi ya wagonjwa wa kifua kikuu jijini Arusha,Tanzania imepanda kwa asilimia 7.5
kwa mwaka 2012-2013.Ongezeko hili linatokana na juhudi kubwa zilizopo
kati wadau mbalimbali wa kupambana na ugopjwa huu katika kuweka wazi
kwa kutoa Elimu inayohusu jinsi ya kujikinga na tiba ya kifua kikuu.
Akizungumza ofisini kwake mapema jana,mratibu wa mapambano dhidi ya ugojwa huu jijini jijinii Arusha Maiko
Kingazi ameeleza kuwa jamii imehamasika vya kutosha katika kutoa
taarifa ya wenye dalili na uelewa juu ya ugonjwa
huu imeongezeka kutokana na Elimu inayotolewa na wadau mbalimbali kwa
jamii.
Tangu awali ulikuwepo ugonjwa huu tatizo lilikuwa kuwapata na kuwatambua waliopata maambukizi ya kifua kikuu jambo ambalo
kwa sasa wananchi wana uelewa mpana hivyo wana jitokeza katika kupima
ili kubaini wameambukizwa au laa.
Aidha kwa upande wake
mratibu wa mapambano dhidi ya kifua kikuu na ukoma jiji la arusha kanda
ya Magharibi Dr Lameki Kaaya amezitaja changamoto zinazoikabili ofisi
yake katika kupambana na ugonjwa wa kifua kikuu mojawapo ikiwa ni kuhama
kwa wagonjwa,ambayo husababishwa na wagonjwa wanaokuja kujtibiwa kutokt
mikoani kutomaliza matibabu kutokana na unyanyapaa unaojitokeza kwa
ndugu na jamaa wanapogundua kuwa ndugu yao ameshapata maambukizi.
Hata hivyo Dr Kaaya alitoa wito kwa jamii na wananchi kwa ujumla kuwa na mazoea ya
kupima afya zao mara kwa mara ili kuweza kubaini tatizo mapema na
kushughulikiwa kwa wakati.
Post a Comment