MTANGAZAJI

VIONGOZI WA DINI WATAKIWA KUSAIDIA VITA DHIDI YA UNYANYAPAA KWA WANAISHI NA VVU

Baraza la Taifa la watu wanaoishi na Ukimwi(NACOPHA) limewashauri viongozi wa dini kuwa mstari wa mbele kusaidia vita dhidi ya unyanyapaa kwa watu wanaoishi na VVU kwenye ibada zao.

Mwenyekiti wa NACOPHA Vitalis Makuyula ametoa ushauri huo hivi karibuni mjini Morogoro wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo na kuondoa unyanyapaa kwa viongozi wa dini na wadau wengine kwa
ufadhili wa shirika la kimataifa la UNAIDS.

Makuyula amesema viongozi hao wa dini wana nafasi kubwa kukutana na waumini na kuwaelimisha namna ya kupambana na Ukimwi na kujiepusha na Unyanyapaa kwa watu wanaoishi na virusi hivyo.

Amesema kwa kuwa viongozi wa dini hukutana na watu wengi mara kwa mara ni vema kuwapatia uwezo zaidi wa kutambua dalili za unyanyapaa na kutoa elimu katika ibada zao.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.