MTANGAZAJI

SERIKALI YA TANZANIA KUCHUNGUZA BIASHARA HARAMU YA WATOTO WA KIKE WANASAFIRISHWA KWENDA CHINA

Serikali ya Tanzania imebaini kuwepo kwa biashara haramu ya kusafirisha watoto wa kike kwenda nchini China kwa lengo la kuwashirikisha katika ukahaba ambao unadaiwa kusababisha kunyanyaswa kwa wasichana hao na wengine kuuawa.

Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa wa Tanzania Bernard Membe amesema serikali itatuma wachunguzi nchini Uchina kuchunguza biashara hiyo.


Hatua hiyo imechukuliwa mwezi mmoja baada ya msichana mmoja Mtanzania kuuawa kikatili katika mji wa Guangzhou nchini Uchina.


Kumekuwa na wimbi kubwa la wasichana kupelekwa katika nchi za magharibi kwa shahuku ya kupata ajira lakini baadhi yao hujikuta pabaya baada ya kuwasili ambapo hunyang'anywa hati zao za usafiri na kulazimishwa kushiriki ukahaba.


No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.