MVUA KUBWA YASABABISHA MAGARI KUKWAMA HUKO HEDARU,KILIMANJARO
Magari yamekwama katika eneo la Hedaru,Same Kilimanjaro baada ya barabara
ya Dar es salaam kwenda Arusha kufungwa na kuzibwa na maji mengi yaliyosababishwa na mvua kubwa
zilizonyesha eneo hilo.Wasafiri wamekwama eneo hili kwani magari na
mabasi na yale ya mizigo yanashindwa kupita kwa kuwa njia haionekani.
Kampuni
ya ujenzi inayojenga barabara hiyo wanajitaidi kuchimba maeneo ya
pembeni ili kuweza kuhamisha maji ili angalau njia iweze kuonekana.Hali
ni mbaya eneo hili hivyo serikali inatakiwa kuwahi kwenda kutoa msaada
wa kuweza kupunguza maji na hatimaye magari yaweze kupita.
Chanzo:DJ SEK BLOG
Post a Comment