MTANGAZAJI

TAMASHA LA UIMBAJI LA VOCAL PRAISE NA GOSPEL FLAMES HILI HAPA

Waimbaji wa Vocal Praise (Pichani) toka katika kanisa la Waadventista Wasabato Magomeni Mwembechai kuanzia leo wakishirikiana na waimbaji wengine wa kanisa hilo Gospel Flames watakuwa wakifanya tamasha la uimbaji kila siku ya ijumaa kanisani hapo kuanzia saa 12:00 jioni hadi saa 1:30 jioni.

Hili litakuwa ni tamasha la aina yake ambapo utasikia nyimbo za injili zilizopangiliwa kiufundi na waimbaji ambao miongoni mwao ni walimu wa kwaya mbalimbali.Hii itakuwa ni changamoto hasa kwa makundi yanayoimba nyimbo za injili za aina ya acappella

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.