TAMASHA LA KURASINI SDA CHOIR DESEMBA 23,2012
Kurasini SDA Choir wanakuletea tamasha kubwa la Injili Desemb 23, 2012 katika ukumbi wa Kilimanjaro ulioko Kilwa Road kwenye viwanja vya maonesho vya Mwalimu Nyerere (saba saba) kuanzia saa sita mchana.
Malengo ya Tamasha hili ambapo kwaya hii itakuwa inatimiza miaka 25 itakuwa ni
·
Kumsifu Mungu kwa njia ya uimbaji
·
Kufanya maombi maalumu ya kumshukuru Mungu kwa
mwaka 2012 na kuombea nchi yetu Tanzania
·
Kuchangia kiasi cha Tsh 80,000,000/= kwa ajili ya
miradi ya kilimo, ufugaji na zahanati kwenye shamba la kwaya huko Bungu- Rufiji
Wageni
mbalimbali wakiwemo wachungaji, Mawaziri, Wabunge na viongozi wengine wa
kiserikali watakuwepo.
Kwaya zingine zitakazokuwepo ni:
·
SUA SDA Choir kutoka Morogoro
·
Temeke SDA Choir
·
Ubungo Hills SDA choir
·
Familia ya Injili
·
Kinondoni SDA choir
Pia watakuwepo-
·
Namsifu Makacha kutoka Arusha
·
Baraka Mchome na Royal Advent kutoka
Morogoro
·
Angel Magoti kutoka Temeke
·
Joseph Oola
Post a Comment