WALIMU MNAKUMBUKA ALICHOSEMA RAIS WA TANZANIA MHE JAKAYA KIKWETE?
HOTUBA YA MHE. DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, KWA WANANCHI, TAREHE 31 JULAI, 2012
Mgomo wa Walimu
"Pengine ni mapema kusema kwa vile kesho Mahakama itaamua kuhusu shauri hilo. Lakini napenda kuwahakikishia walimu kuwa tunawajali, tunawathamini na kutambua mchango wao muhimu kwa taifa letu. Wakati wote tumekuwa tunashughulikia madai ya haki zao na malimbikizo mbalimbali.
Madai ya safari hii ni makubwa mno, yametuzidi kimo. Athari za kuyatimiza yalivyo yataifanya bajeti ya Serikali kutumia asilimia 75 kwa ajili ya mishahara ya watumishi wa Serikali na kubakiza asilimia 25 kwa kuendeshea Serikali na kutimiza majukumu ya maendeleo kwa wananchi. Haitakuwa sawa. Ndiyo maana tumeshindwa kuelewana walipokataa rai hiyo na wao kusisitiza kugoma.
Wakati tunaendelea kusubiri uamuzi wa Mahakama, nina maombi mawili kwa walimu: Moja, wasiwalazimishe walimu wasiotaka kugoma wafanye hivyo, wawaache waendelee na kazi. Pili, wasitumie watoto isivyostahili kujenga hoja zao. Nawasihi warudi kwenye meza ya mazungumzo"
Post a Comment