MTANGAZAJI

RAIS JAKAYA KIKWETE ATEUA MSAIDIZI WAKE

 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete amemteua BIBI MWANAHAMISI OMARI KITOGO kuwa MSAIDIZI WA RAIS,HUDUMA ZA JAMII.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Y.

Sefue leo, Jumanne, Mei 8, 2012, mjini Dar es Salaam inasema kuwa
uteuzi huo umeanza Mei Mosi, mwaka huu, 2012.

Kabla ya uteuzi wake, Bibi Mwanahamisi Omari Kitogo alikuwa Mkadiriaji

Ujenzi Msaidizi (Assistant Quantity Surveyor) katika Kampuni ya COWI,
Tanzania.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.Dar es Salaam.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.