MTANGAZAJI

SHERIA MKONONI-WAWILI WACHOMWA HADI KUFA

Pichani ni miili ya watu wawili wanaodaiwa kuwa majambazi  ambao walipigwa na  kuchomwa moto hadi kifo katika eneo la Ruhuwiko manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.

Baadhi ya wakazi wa eneo la Ruhuwiko ambao hawakutaka kutaja majina yao walidai kuwa kabla ya tukio hilo watu hao hawakuweza kufahamika majina yao waliwasili eneo hilo majira ya saa tatu asubuhi wakiwa na lengo la kuuwa na kuondoa viungo vya uzazi vya binadamu ambavyo inadaiwa vinauzwa kwa fedha nyingi.


Wananchi hao walidai kuwa watu hao walifika kwa mama mmoja ambao walidai wanamtafuta hatimaye wakiwa wanakunywa katika klabu moja ya pombe za kienyeji inadaiwa wakazi wa eneo hilo waliwatilia mashaka watu hao na kuaanza kuwahoji ambapo inadaiwa baada ya kupata kipigo na kuanza kuchomwa walieleza kwamba wao ni wauaji na walipewa fedha kwa ajili ya kuuwa na kwamba tayari wamekuwa wamefanya matukio kadhaa ya mauaji .

Chanzo cha habari kimebainisha kuwa wauaji hao walidai kuwa wapo 50 na wanatakiwa kuuwa watu zaidi ya 100 wakiwemo wanaume 60 na wanawake 40 kwa kuwaondoa sehemu zao za siri ambazo inadaiwa ni biashara ambayo inawapatia fedha nyingi .

Baada ya wauaji hao ambao walikutwa na shilingi 500,000 kukiri kuwa kazi yao ni kuuwa ndipo wananchi wengi wenye hasira waliamua kuanza kuwapa kipigo kizito kisha kununua petroli na kuanza kuwachoma wakiwa hai .Hadi polisi wanafika katika eneo hilo miili ya watu hao ilikuwa inaendelea kuungua kwa moto.

Uchunguzi umebaini kuwa wakazi wa Ruhuwiko waliamua kuchukua sheria mkononi baada ya matukio ya uharifu na  mauaji kujitokeza katika eneo hilo  na kwamba hii ni mara ya pili kwa wakazi wa Ruhuwiko kufanya mauaji ya kutisha ambapo miaka 25 iliyopita watu wengine wawili waliodaiwa kuwa ni majambazi sugu waliuwa na kisha miili yao kuchomwa moto.

"Mimi binfasi nimefurahia sana kitendo hiki labda sasa majambazi yataogopa kuendelea kufanya uharifu katika eneo hili,hivi sasa hatuna amani kabisa wizi imekuwa ni jambo la karibu kila siku ,mauaji nayo yanazidi kuendelea ,waharifu wengine wanakamatwa na kuachiwa  acha wananchi wajichukulie sheria mkononi'',alisema mama mmoja ambaye hakutaka jina lake kuandikwa.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na polisi bado wanaendelea na uchunguzi.

Chanzo : Haki Ngowi Blog

1 comment

Yasinta Ngonyani said...

Sheria, Sheria. Sheria ipo wapi? hii yote inatokana na kwamba watu wengi wamekuwa wakifanya kosa na wakikamatwa wanaachiliwa na kuendelea kufanya kosa tena. Ndio maana watu wanaamua kujichukulia sheria mkonon. Lakini pamoja na hili si haki kwa kweli.

Mtazamo News . Powered by Blogger.