USO KWA USO NA WAZIRI MKUU WA TANZANIA KUPITIA STAR TV
Mh Waziri MKuu wa Tanzania Mizengo Pinda akifanya mahojiano na Baraka Baraka nchi Uingereza |
Salam,
Urban Pulse Creative wakishirikiana na Star tv wanakuletea Mahojiano Maalum na Mh. Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipofanya ziara nchini Uingereza hivi karibuni. Mahojiano haya yalikuwa yamelenga zaidi kupata ufahamu na uchambuzi wa namna serikali yetu ya Tanzania inavyofanya kazi pamoja na changamoto zake.
Mbali na hapo tulijadiliana kuhusu Majukumu ya Waziri mkuu, Chakula, Nishati, Jumuiya ya Afrika Mashariki na mchakato wa katiba Mpya kuelekea kuazimisha miaka 50 ya uhuru.
Mahojiano haya yalifanywa na Baraka Baraka Kutoka Urban Pulse na yatarushwa Hewani kupitia kituo cha Star TV Jumapili ijayo Tarehe 30 octoba 2011 kuanzia saa 10.30 katika kipindi cha Medani za siasa.
Tafadhali usikose kuangalia kipindi hiki ili upate kujifunza mambo mbalimbali kuhusu Tanzania na Serikali yetu.
Asanteni,
Frank Eyembe-Urban Pulse Creative
Post a Comment