MTANGAZAJI

DAR ES SALAAM SI SAFI


1.       Jiji la Dar es Salaam limekubuhu kwa uchafuzi wa mazingira hali iliyofanya wakazi waishio humo kushangaa kuitwa jiji kutokana na kero za uchafuzi wa mazingira ambao ungeweza kuzuilika kukua siku hadi siku.
 Dar es Salaam imekuwa iko shagala bagala katika mitaa yake ya jiji hali inayofanya kukosa hadhi ya kuitwa jiji kutokana na mazingira yake hayaridhishi machoni mwa watu


Mazingira yamekuwa hovyo kwa baadhi ya mitaa ya jiji kwa kuonekana kwa baadhi ya wakazi kushindwa kudumisha suala la usafi wa mazingira wanayowazunguka.


Jiji hilo hali huwa mbaya zaidi hasa pindi mvua zinaponyesha na wakazi hao kuacha uchafu wa vyooni, mitaro kutirrika barabarani hali inayofanya uchafunzi wa mazingira uzidi kuongezeka.
Mamlaka husika wa afya na usafi wa jiji pia wameonekana kuchangia kwa asilimia kubwa uchafuzi huo wka kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo


Hivi sasa wafanyabiashara ndogondogo wamekuwa wakijiendeshea shughuli zao mahali popote wanapojisikia na sehemu ambazo si rasmi na kufanya kuacha taka ngumu katika maeneo ya jiji na mamlaka husika kufumbia macho suala hilo na inasikitisha majalala ya kutupia taka yakiwa katikati ya barabara, kati ya nyumba na nyumba hali inayofanya uchafuzi wa mazingira na ili hali mamlaka hizo kutumia mamilioni ya fedha za walipa kodi kushughulikia taka hizo hizo

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.