MTANGAZAJI

WAZIRI MKUU WA TANZANIA MIZENGO PINDA AONGEA NA URBAN PULSE


Waziri Mkuu wa Tanzania Mh.Mizengo Kayanza Pinda akijibu maswali kutoka kwa Baraka Baraka
 
Salam,
URBAN PULSE CREATIVE  Ilipata fursa ya kufanya mahojiano maalum na MH Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipokuja katika Ziara yake hapa nchini Uingereza siku chache zilizopita. Mahojiano hayo maalum yalilenga zaidi kuelemisha jamii yetu ya kitanzania, vile vile kutoa Msimamo kutoka katika serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusiana na mambo mbalimbali yanayomhusu Mtanzania .
Mahojiano hayo yaligusa maeneo tofauti yakiwepo majukumu pamoja na changamoto anazokumbana nazo Mh waziri mkuu, Suala la katiba, Uchumi, Rushwa na Ufisadi,  Miundo Mbinu, Maendeleo, Chakula, Nishati, Jumuiya ya Africa mashariki pamoja na mambo mengine mengi.
Mahojiano yalifanywa na Baraka Baraka Kutoka URBAN PULSE CREATIVE MEDIA na yatarushwa hewani mda sio mrefu.
MUNGU IBARIKI AFRICA, MUNGU IBARIKI TANZANIA
Asanteni,
URBAN PULSE CREATIVE MEDIA-UINGEREZA

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.