MTANGAZAJI

ZIARA YA BALOZI WA TANZANIA UK KUTEMBELEA MJI WA READING

Mh Balozi Peter Kalllaghe
Salaam,

JUMUIYA YA WATANZANIA- TANZ-UK Inapenda   kuwatangazia  watanzania wote waliopo  Reading, Slough, Oxford  na vitongoji vingine vya karibu  kuwa Imeandaa ziara maalum ya Mheshimiwa  Balozi  Kallaghe  ya siku tatu itakayofanyika katika  mji wa Reading kuanzia tarehe 8-10/4/2011.

Sambamba ya ziara hii Mh Balozi atapata fursa ya kutembelea  shughuli mbalimbali za kimaendeleo zifanyazwo na  wajasilimali wa kitanzania na pia kukutana na wanajumuia wote.
Hivyo basi kutakuwa na sherehe maalum ya kumkaribisha Balozi wetu hapa Reading tarehe 9/4/11 kuanzia saa 10 jioni mpaka saa 12 jioni baada ya hapo kutakuwa na tafrija pamoja na mziki kuanzia saa 1 usiku mpaka saa 6 usiku. 

Tafadhali wahi mapema Ukumbi  na adreess ya kwenye sherehe
 Amersham Road Youth & 
Community CentreAmersham Road,
Caversham,
Reading,
Berks,
RG4 5BP

Tunawomba watanzania wote mjitokeze kwa wingi ili kumkaribisha Balozi wetu. Kuja kwenu ndio kufakisha kwa ziara hii muhimu, tafadhali mjulishe mwenzio.
Ratiba Rasmi ya ziara kamili itatolewa baadaye.
Asanteni kwa ushirikiano wenu,
Mwenyekiti
Tanz- UK

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.